How to start a successful poultry farm in kenya
Ufugaji wa kuku ni biashara ambayo inaweza kubadilisha maisha ukifanywa kwa mpango na nidhamu. Huku Kenya mahitaji ya mayai na nyama ya kuku yanaendelea kuongezeka kila siku. Ukiingia kwa mchezo unaweza kukata tamaa mapema, lakini ukiingia ukiwa na plan safi na malengo ya kueleweka unaweza kuona matokeo mazuri. Kitu ya kwanza ni kuelewa soko, kuchagua aina ya kuku unaotaka kufuga, na kuhakikisha una nafasi nzuri ambayo ni salama na safi. Hapo ndio foundation ya biashara yenye nguvu inaanzia. Usikimbilie kununua kuku wengi ukiwa bado hujajipanga. Anza na idadi ambayo unaweza kusimamia vizuri halafu ukue pole pole kadri biashara inavyozidi kushika. Chagua vifaranga kutoka kwa hatchery zinazojulikana ili upate stock yenye afya. Wape chakula bora, maji safi kila wakati, na hakikisha banda lina hewa ya kutosha. Hapo ndio kuku wako watagrow poa na kupunguza losses ambazo huumiza pocket. Health ya kuku ni deal kubwa sana. Ratiba ya chanjo inafaa kufuatwa bila mchezo na banda lisafishwe ...